Mamlaka ya dawa na vifaa tiba kupitia kwa mkurugenzi wa mamlaka hiyo Adam Fimbo, amesema kwamba ni marufuku abiria kununua dawa mbalimbali hasa za kutibu magonjwa zinazouzwa kwenye magari na vyombo vingine vya usafiri nakusema kwamba endapo mnunuzi na muuzaji watakamatwa watachukuliwa sheria.
Mkurugenzi huyo amesema kabla yakutumia dawa inapaswa mtu kupata ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja nakupata vipimo.