Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewataka wafanyabiashara hasa wa gesi ya kupikia majumbani kubuni mbinu za kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini ili waweze kumudu gharama za nishati hiyo mbadala.
Hiyo ni kutokana na kile kilichobainishwa kuwa Watanzania wengi bado wanatumia mkaa na kuni kama vyanzo vya kupikia jambo ambalo linachangia uharibifu wa misitu.
Amesema licha ya uwepo wa baadhi ya nishati mbadala ambazo watu huweza kuzitumia kama vyanzo vya kupikia lakini ukuaji wa matumizi wa nishati hizo ni wa asilimia mbili tu kwa mwaka.
“Tatizo kubwa lililo mbele yetu ni namna gani unapunguza bei ya nishati mbadala na bei ya majiko, sasa naomba niwasihi vyuo vyetu na vinginevyo, watafiti ni nini kinasababisha bei ya nishati mbadala na vifaa husika kuwa kubwa na nini kifanyike.” Mpango
“Kama ni kuangalia mfumo wa kozi basi tuutazame lakini pia kama ni gharama za kuzalisha nishati mbadala nazo ziweze kutazamwa,” Mpango