Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Sh2.3391 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo.
Hayo yamesemwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Dkt. Mwigulu amesema mradi iliyopitiwa fedha hizo ni ya uboreshaji wa barabara za vijijini na fursa za kijamii (RISE), mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (Heet).
Miradi mingine ni wa kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za mtandao (DTP) na mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za Umeme Zanzibar (Zesta).