Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewaelekeza Wataalamu wa Lishe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha kila Shule inakuwa na kibao maalum cha kupima urefu wa Mtoto ili kutambua mwenendo wa makuzi yake.
Ametoa maelekezo hayo leo Dodoma alipokutana na timu ya mradi wa boresha lishe kutoka WFP unaofadhiliwa na EU na kutekelezwa kwa miaka mitano 2017 hadi Juni 2021 Mikoa ya Dodoma na Singida.
Lengo la upimaji huo ni kuufuatilia udumavu wa Watoto na kubaini lishe wanayoipata majumbani ili kufanya ufuatiliaji———“Mtoto mwenye lishe duni na aliyedumaa tutambaini tu kupitia urefu wake, mkakati huu ni kwa Watoto wote waliomaliza muda wa Kliniki”
Waziri Mhagama ameiomba pia Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia SIDO na VETA kutengeneza vibao vya kupima makuzi ya Watoto kwa kila Mkoa.