Hadi kufikia sasa, Tanzania ina jumla ya watumiaji Milioni 29 wa huduma za intaneti kupitia simu za mkononi, huku idadi ya laini za simu ikifika Milioni 53.1.
Vilevile, asilimia 26 ya watu takriban Milioni 60 hapa nchini, ndio pekee wanaomiliki simu janja hadi kufikia mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia moja kutoka asilimia 25, iliyokuwepo Julai 2020.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile, amesema takwimu hizo ni rasmi.
Dk. Ndugulile amesema kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kati ya laini Milioni 53.1 zilizosajiliwa kisasa (kwa alama za vidole), Milioni 32.7 pekee ndizo zinatumia huduma za fedha mtandaoni.
Hata hivyo, amesema takwimu hizo za TCRA zinabainisha kuwa uwiano wa mawasiliano ya simu kwa wananchi kupitia kasi ya 2G hadi Machi mwaka huu, ilifikia asilimia 93 ya idadi ya watu nchini.
WOSIA WA TB JOSHUA KUELEKEA BIRTHDAY YAKE “HAITAKUWA RAHISI, SITOWEZA KUSHEREHEKEA”