Marais 100 wa zamani wa Nchi mbalimbali duniani pamoja na Mawaziri wa zamani wakiwemo Mawaziri Wakuu wamelihimiza kundi la Mataifa 7 tajiri duniani – G7 kulipia kampeni za chanjo ya corona Duniani ili kuzuia virusi kubadilika na kurejea kama kitisho cha Ulimwengu.
Viongozi hao wametoa ombi lao kabla ya mkutano wa kilele wa G7 nchini England ambao utaanza Ijumaa wiki hii ambapo Rais wa Marekani Joe Biden atakutana na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Canada na Japan.
Katika barua yao kwa G7, Viongozi hao wa zamani wamesema ushirikiano wa kimataifa umeshindwa katika mwaka wa 2020 lakini 2021 unaweza kuleta enzi mpya, miongoni mwa Viongozi waliotia saini zao ni Mawaziri wakuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown na Tony Blair, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Viongozi wa zamani 15 wa Afrika.
WOSIA WA TB JOSHUA KUELEKEA BIRTHDAY YAKE “HAITAKUWA RAHISI, SITOWEZA KUSHEREHEKEA”