Rais Museveni amepiga marufuku mikusanyiko yote nchini Uganda ikiwemo ibada za pamoja Misikitini na Makanisani kwa muda wa siku 42 hii ni kufuatia wimbi la pili la Corona kuleta athari kubwa nchini Uganda ukilinganisha na wimbi la kwanza.
“Kwenye wimbi hili kiwango cha Watu kufariki ni kikubwa kuliko tulivyotarajia na Wagonjwa wanaozidiwa ni wengi, kwenye Wimbi la kwanza ilituchukua miezi 3 hadi 4 kufikia kuwa na hali mbaya lakini sasa ni wiki mbili tu mambo magumu, vifo vimefikia 374, wagoniwa 52,929”———Museveni
“Watu nwasitembee kuanzia saa tatu usiku hadi 11 Alfajiri, mikusanyiko marufuku isipokuwa kwa shughuli za Kimahakama au za Kibunge, mkikaidi masharti nikirudi tena hapa natangaza lockdown (hakuna kutoka ndani iwe mchana au usiku)”———Museveni
WOSIA WA TB JOSHUA KUELEKEA BIRTHDAY YAKE “HAITAKUWA RAHISI, SITOWEZA KUSHEREHEKEA”