Mkuu wa Mkoa wa DSM Amos Makalla amefanya kikao cha pamoja na watumishi wa Mkoa huo kwa lengo la kuweka mipango ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa maslahi ya wananchi na kuwapatia agenda tano za kufanyia kazi.
Miongoni mwa agenda alizotoa Rc Makalla ni Ulinzi na Usalama wa Wananchi ambapo amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya kuhakikisha wanashusha suala hilo ngazi ya Kata na Mitaa ili kumaliza kabisa matukio ya uhalifu.
Aidha RC Makalla amewataka viongozi wote wa Mkoa huo kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini kuhakikisha suala la usafi wa mazingira inakuwa ni agenda muhimu na kutoa wito kwa wananchi kusafisha mazingira wanayoishi ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Pamoja na hayo Rc Makalla amehimiza Suala la ukusanyaji wa mapato ambapo ametaka mkoa huo kuendelea kuwa kinara wa ukusanyaji wa mapato kwakuwa umekuwa ndio mchango mkubwa kwenye kuchangia pato la Taifa.
Hata hivyo RC Makalla ametaka kila Mkuu wa Idara kuhakikisha anajua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye idara yake na kuisimamia ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora uliopangwa.
Sanjari na hayo RC Makalla pia ametaka Watumishi kusikiliza kero na changamoto za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akizikumbusha Halmashauri kuhakikisha zinatekeleza takwa la kisheria kwa kutenga asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, Walemavu na wanawake.
MAPYA YA MKUDE NA SIMBA, HUKUMU YAKE MPAKA ATOKE MUHIMBILI