Watu wanne wamekamatwa nchini Marekani akiwamo Padre Fidelis Moscinski kutoka Shirika la Wakatoliki la Wafransiska –CFR baada ya kuandamana kuelekea katika kliniki ya Cuyahoga Fall ambayo ni maalumu kwa utoaji mimba nchini humo.
Padre huyo na wenzie waliandamana kupinga utoaji wa mimba kwenye Kliniki hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuanza kusali kando ya majengo ya kliniki hiyo kabla ya kukamatwa na polisi wa Mji wa Ohio.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa mji huo, washtakiwa hao wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya manispaa ya Stow.
Washtakiwa hao wanne ambao ni Padre Fidelis Moscinski mwenye umri wa miaka 51, Laura F. Giles – 56, Audrey S. Whipple – 18, na Clara S. McDonald – 62, wanaweza kufungwa jela kwa siku 30 au kulipa faini ya zaidi ya Sh milioni moja.