Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya operesheni dhidi ya magari mabovu ambayo hayapaswi kuwepo barabarani rasmi kesho, ili kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya moto na kuepuka ajali za barabarani.
“Nimeelekeza operesheni ya usalama barabarani, kuna makosa ya barabarani yameanza kujitokeza kama mnavyoona ajali iliyotokea Mbeya, Shinyanga, operesheni dhidi ya magari mabovu nayo itaanza kesho, nawaambia ma RTO, wakuu wa matraffik mikoa yote kufanya operesheni dhidi ya magari mabovu ambayo hayatakiwi kuwepo barabarani” IGP Sirro
“Wananchi wa Dar es Salaam wametoa ushirikiano mkubwa sana kwa jeshi la polisi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, silaha nyingi zimekamatwa wahalifu wengi wamekamatwa, nimeongea na wenyeviti wa mtaa na watendaji Kata wote wa Dar es Salam, tumekuwa na mafanikio makubwa nafikiri wana Dar es Salaam wameona, leo tunahitimisha operesheni lakini tunaanza operesheni nyingine tena ya mwezi mzima na ni nchi nzima” IGP Sirro
UWEZO WA MTOTO WA UWOYA KUCHEZA MPIRA “BABA NA RONALDO WANANIVUTIA UWANJANI”