Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya MeLT, Fatema Dewji ametoa wito kwa Watanzania kutumia vifaa vya kielektroniki kutoka kampuni ya LG kwa kuwa ni vifaa ambavyo rafiki kwa mazingira.
Dewji ametoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa duka la pili la kampuni hiyo ya LG Electronics lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo alisema MeLT inashirikiana na LG katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki kutoka LG hapa nchini ambavyo ni pamoja na runinga, mashine za kufua nguo, friji na vifaa vingine.
“Vifaa hivi vina ubora wa juu lakini pia vinatumia teknolojia mpya ambayo inatumia umeme mdogo na rafiki kwa mazingira ndio maana hata sasa tunaona kuwa Watanzania wamekubali bidhaa za LG hii ina maanisha kuwa Tanzania kuna soko kubwa” alisema.
Kauli hiyo ya pia iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Mauzo wa MeLT, Hussein Dewji ambaye alitoa wito kwa Watanzania kutembelea maduka hayo ya LG ili kujionea bidhaa bora na kufanya uamuzi sahihi katika ununuzi wa bidhaa za majumbani mwao.
Aidha, Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim alisema duka hilo ni pili hapa Tanzania baada ya juzi kuzindua duka la kwanza katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar.
“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzanaia yalivyochangamka. Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu”
“Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza. Tutawapa wafanya biashara wa Tanzania fursa nzuri ya kufanya kazi na sisi mfano mzuri ukiwa ni MeTL ambaye ni msambazaji mkuu wa bidhaa zetu za LG hapa Tanzania pamoja na dealers kama F&S ambaye ni mfanyabiashara wa kwanza katika mpango wetu wa thamani wa Tanzanite Club Tanzania” alisema Kim.
Kwa upande wake Henry Chami ambaye ni mwakilishi kampuni ya F&S inayojishughlisha na uuzaji na usambaji wa bidhaa za kielekroniki, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja Watanzania watapa fursa ya kununua bidhaaza LG katika dula hilo la Mlimani City kwa bei punguzo hadi asilimia 25.
“Ofa hiyo inalenga kutoa motisha kwa Watanzania kupata bidhaa bora za LG kwa sababu mbali na ubora na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika kutengeneza pia upatikanaji wake ni wa urahisi zaidi,” alisema.