“Mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja ambapo ulipungua kutoka wastani wa 3.4% mwaka 2019 hadi 3.3% mwaka 2020, mfumuko wa bei umebaki katika wigo wa 3.3% Mei 2021″ Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendelo wa Taifa wa mwaka 2021/22
“Mwenendo wa mfumuko wa bei umeendelea kuwa tulivu kutokana na upatikanaji wa chakula cha kutosha, kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani na sarafu nyingine duniani na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti”———Nchemba
“Hadi Aprili 2021, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 60.9, ikilinganishwa na shilingi trilioni 55.5 kipindi kama hicho mwaka 2020, kati ya ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi trilioni 43.7 na deni la ndani ni shilingi trilioni 17.3, ongezeko hilo lilitokana na kupokelewa kwa fedha za mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo”———Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba
“Taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2020 inaonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa”———Waziri Mwigulu akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendelo wa Taifa wa mwaka 2021/22