Rawan Dakik ni msichana wa kitanzania ambaye amevunja rekodi kwa kufika kwenye kilele cha mlima mrefu zaidi duniani wa Everest nakushika rekodi ya msichana mwenye umri mdogo zaidi Afrika wakupanda mlima huo nakufika kileleni
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 20 ametua nchini Tanzania akitokea nchini Nepal ambapo amepokelewa na naibu waziri wa maliasili na utalii Mary Masanja akiambatana na viongozi wengine akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela
Rawan Dakik amesema anafurahi kufika Tanzania licha ya changamoto alizokutana nazo wakati akipanda mlima huo
“Nimepita changamoto na hatari nyingi katika safari yangu lakini kilichonipa nguvu niliona nina wajibu wakulipa Taifa langu la Tanzania heshima yakufika kilelele cha mlima mrefu duniani nikiwa msichana mdogo Africa,nafurahi bendera yangui imerudi Tanzania na nafurahi sana”-Rawan
HII NDIO GARI AINA YA FIAT, NI BALAA INA GIA TISA INABEBA MZIGO MKUBWA, DEREVA AIELEZEA