Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza wito wake kuwa Majaji sita walioachwa kwenye orodha ya wale walioteuliwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni lazima wateuliwe .
Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Daniel Musinga kama Rais wa Mahakama ya Rufaa, amesema wakati huo ulikuwa mchungu, kwa sababu Majaji wanne ambao waliteuliwa kwa korti ya Rufaa walikuwa bado hawajateuliwa.
Koome amesema Mahakama iko katika hatari ya kutekwa na idara na vile vile “watu ambao sitawataja”.
Koome pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu ufadhili mdogo wa Mahakama na akamuambia Spika wa Bunge la taifa Justin Muturi moja kwa moja, akisema kwamba mgao wa Sh37 bilioni ulikuwa mdogo sana kati ya Bajeti ya Sh3.6 trilioni iliyosomwa siku Alhamisi.
Koome alisema Idara ya Mahakama ilikuwa ikifanya kazi katika “jumba la makavazi” ambalo lilikuwa katika hali mbaya na akashangaa kwa nini wizara ya Afya haijalitaja jengo hilo kama hatari ya kiafya lisilofaa kutumiwa