Mamlaka ya Anga Nchini Marekani imetangaza faini za maelfu ya dola kwa Abiria mbalimbali ambao walileta ukorofi ndani ya Ndege Nchini humo huku ikisema kesi hizo za Abiria kwenye Ndege zimezidi elfu tatu toka mwaka 2021 uanze.
Faini walizotozwa ni kama ifuatavyo ambapo Abiria Mwanamke alieingiza kidole chake puani na kumtukana Muhudumu wa Ndege na kusababisha Ndege hiyo kutua kwa dharura kisa ugomvi wake wa kukataa kutii agizo la kuvaa mask alilopewa na Muhudumu huyo anakabiliwa na faini ya USD 10,500 (Tsh. milioni 24+)
Abiria mwingine ambaye alikataa kutii agizo la Muhudumu wa Ndege aliyemkumbusha karibu mara kumi kuvaa barakoa (mask) na kukutwa akinywa pombe ambayo haikutoka kwa Wahudumu wa Ndege hiyo ametozwa kulipa faini ya USD 15,500 ambazo ni zaidi ya Tsh. milioni 35.
Abiria mwingine wa Ndege ya Alaska kutoka Boise, Idaho kwenda Los Angeles ambaye alikutwa kwenye choo cha ndege akivuta sigara ya kielektroniki (e-cigarette) na wakati huohuo kukataa kutii agizo la Muhudumu wa Ndege aliyemkumbusha kuvaa barakoa (mask) amepigwa faini ya USD 10,300 ambayo ni Tsh. milioni 23.8 huku faini ya Abiria mkorofi aliyetaka kufungua mlango wa ndege wakati ikiwa angani ikitajwa kuwa USD 52,000 ( zaidi Tsh. milioni 120 ).