Mahakama Kuu ya Tanzania imeqaachia huru Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake. Ayo TV na Millardayo.com imezungumza na Wakili wa washitakiwa hao Juma Nassoro.
‘Ni kweli tumepata taarifa ya kustukiza ni kwamba masheikh wameanza kuachia kuanzia usiku wa jana, kwa maana ya kesi ilipokuwa imefikia tayari mara ya mwisho tulipokuwa mahakamani walisomewa mashtaka yao baada ya kufanikiwa kuyaondoa mashtaka 14 kati ya 25 kwenye pingamizi tuliyokuwa tumeyaweka’-Juma Nassoro
‘Na sasa yaliyokuwa yamebaki mashtaka kumi na moja walisomewa na waliyajibu kwa kuyakanusha kuwa si kweli na hatua ya pili yaliyafanyika maelezo ya awali ambapo kila mmoja alihusika wapi na waliyajibu na kuyakanusha sasa baada ya hapo kesi ikawa imeahirishwa kwamba itapangwa tena tarehe nyingine ambapo tutaitwa mahakamani tayari kwa upande wa Jamhuri kuwaita mashahidi wao‘-Juma Nassoro
‘Sasa wakati tunasubiria hao mashahidi wa Jamhuri tuone watakachokileta mahakamani sasa jana usiku nilipigiwa simu nakuambiwa kwamba swala imeswalishwa na Sheikh Faridi pamoja na sheikh Msele Mwali na ilipofika asubuhi ilibidi tufuatilie kwa kina tukakutana kwamba ni kweli masheikh wawili wameachiwa na wengine wanaendelea kuachiwa kidogo kidogo’_Juma Nassoro
‘Najua kutakuwa na swali ya mbona yamekuwa ghafla ni wanaachia katika mazingira haya ikumbukwe wenye kesi ni Jamhuri dhidi ya hawa Masheikh ninafikiri kwa kile kilichoendelea pale Mahakamani pengine wameona sasa kwamba hawana kesi ndio maana wakaona waiondoe ama wameamua kuwasamehe’- Juma Nassoro