Mwasisi wa Taifa la Zambia Kenneth Kaunda amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu ya maradhi ya Pneumonia, Kaunda amefariki akiwa na umri wa miaka 97.
Watoto wake wa kiume Panji na Kambarage Kaunda wamethibitisha, siku tatu zilizopita Kaunda alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Kijeshi mjini Lusaka.
Maafisa hata hivyo hawakuweka wazi maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, lakini baadaye yalibainika kuwa ni Pneumonia wakati Taifa hilo la kusini mwa Afrika likishuhudia kuongezeka kwa maambukizi ya maradhi ya COVID-19.
Kaunda alikuwa akichukuliwa kama mmoja ya manusura wa mwisho miongoni mwa kundi la mashujaa wa uhuru barani Afrika, alitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi 1991.