Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwakuwa Watu wameshindwa kutekeleza maagizo ya kutotembea mitaani kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11:30 Alfajiri, anakaza zaidi masharti ya Corona na kuanzia sasa ni marufuku Mtu kutembea usiku kuanzia saa moja usiku hadi 11:30 Alfajiri.
“Shule na Taasisi za Elimu ya Juu zitaendelea kufungwa kwa siku 42, Uwanja wa Ndege wa Entebbe utaendelea kufanya kazi lakini tutahahakisha hakuna kirusi kipya kinaingia Uganda” Museveni
“Viwanda havitofungwa lakini penye uwezekano sio mbaya kwa Wafanyakazi wakaruhusiwa kuishi kiwandani kwa siku 42 kuzuia kutoka na kuingia, lengo ni kupunguza maambukizi ili tuweze kuwatibu wachache usipofanya hivyo utaanza kuingia kwenye ligi ya kuchuana na USA, Italy na India na wengine kwa maambukizi makubwa ya Corona” Museveni
“Ili maisha yetu yaweze kuendeea sekta zifuatazo hazitofungwa, kilimo, viwanda vya uzalishaji, Utaliii, usafirishaji wa mizigo, ulinzi, maduka ya rejareja, huduma za afya na idara za matibabu” Museveni