Mwanamke mmoja aitwae Kanok Wan wa Bangkok Thailand amekamatwa na Polisi baada ya kuichoma moto pikipiki ya EX-Boyfriend wake kutokana na Mwanaume huyo kukataa warudiane.
Video iliyorekodiwa na camera za usalama kwenye jengo ilimuonesha Mwanamke huyo akiiwasha moto baada ya kuimwagia petroli iliyokua kwenye dumu ambapo taarifa zaidi imesema thamani ya pikipiki hiyo ni ( $ 31,000) ambayo ni Tsh. milioni 71.8.
Wan mwenye umri wa miaka 36 alimnunulia Boyfriend wake pikipiki hiyo kama zawadi wakati penzi lao likiwa limetaradadi lakini walipogombana na Boyfriend kukataa kurudisha penzi ndio akaipiga kiberiti na baada ya kufanya hivyo camera za jengo hilo zimemuonesha akiiondoka kwa kutumia gari jekundu alilokua amelipaki nje.
Wan amesababisha hasara sio tu ya pikipiki ya EX-Boyfriend wake bali pikipiki nyingine sita zilizokua karibu na pikipiki hiyo ambazo zote zimeteketea kwa moto.