Baadhi ya mawakala wanaofanya biashara ya fedha kwenye maduka mkoani Arusha wamezungumzia aina ya wizi mpya unaodaiwa kuibuka ambao hupiga simu kwenye maduka hayo nakudai kwamba wao ni mawakala wakuu nakuwataka kufuata maelekezo wanayowapa huku wengine wakitumia njia nyingine mbalimbali ambapo ndani ya miezi miwili zaidi ya wateja wanne wameshaibiwa.
Raimu Said ni kijana ambaye anadai kutapeliwa million nne wiki iliyopita anasema alipigiwa simu na watu waliojitambulisha kwamba ni wakala mkuu nakumtaka abonyeze namba walizomtajia ikapelekea kubadilisha mfumo wa simu alizokuwa nazo ambapo alituma million nne baada ya kutaja kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye simu anazo fanya nazo biashara
“wakati naongea nao wakanipa maelekezo wakaniuliza kuhusu cammision ,wakaniambia niwape namba zangu nikawapa baada ya hapo wakawa wananitajia namba kumbe nilikuwa natuma pesa wakaniuliza una kiasi gani nikawataja”-Raimu Said
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema wamekuwa na kitengo kinachohusiana na makosa ya kimtandao na kuhusu wizi wa kwenye maduka ya mawakala atalifanyia kaz nakuwataka watu kuwa makini na matapeli hao