Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limeanzisha ukaguzi wa mabasi na malori yanayoingia na kutoka Mkoani humo, huku likiyafungia mabasi 15 kusafirisha abiria, baada ya kuyabaini kuwa ni mabovu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stellah Mutabihirwa, amesema ndani ya mwezi mmoja wa Juni 2021, Jeshi hilo limekagua magari makubwa zaidi ya 1,900, yakiwemo mabasi 223, na baadhi yameonekana kuwa mabovu, hali inayohatarisha usalama wa abiria.