Serikali imetenga Bilioni 2.07 kwa ajili ya kupatiwa umeme wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili kwa Vijiji vyote ambavyo havijapata umeme katika katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, amesema utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.
Dk. Kalemani alikuwa akijibu swali na Mbunge wa Arumeru Mashariki John Pallangyo, aliyehoji ni lini Serikali itawasha umeme kwenye vijiji na vitongoji vyote katika Jimbo la Arumeru Mashariki ambavyo umeme bado haujawashwa.?
Dk Kalemani alisema vitongoji vya Jimbo la Arumeru Mashariki ambavyo havijafikiwa na umeme vitaendelea kupatiwa umeme kupitia mradi wa ujazilizi (Densification) unaotarajiwa kuanza mwezi Julai, 2021.
Aidha, alisema kazi ya kupeleka umeme katika vitongoji ni endelevu, Serikali kupitia TANESCO na REA itaendelea kupeleka umeme katika vitongoji kulingana na upatikanaji wa fedha.
MZEE AFUNGUKA KWA HISIA MBELE YA DC GONDWE “HATUKUTAKA KUJA HAPA, NASI TUNASHUKA HUKOHUKO”