Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”
“Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza”———M/kiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
“Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu”———MBOWE
“Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru” ——M/kiti wa CHADEMA,Mbowe