Stori ya shabiki aliyerushia ndizi Alves imekua ni stori kubwa ambayo imepokelewa na mataifa mbalimbali duniani huku wengi wakionekana kumuunga mkono Alves,Polisi nchini Uhispania,wamesema wamemkamata shabiki yule aliyemtupia ndizi mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya Jumapili akiwa uwanjani.
Dani Alves ambaye ni raia wa Brazil anayechezea soka lake katika klabu ya Barcelona ambacho Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili.
Kitendo alichofanya Alves ni kuchukua Ndizi hiyo na kuila,tukio ambalo limemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii,Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha,Alvesi amesema ameshangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.
Katika mechi hiyo Barcelona walishinda Villareal mabao 3-2 katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa El Madrigal mjini Castellon pwani ya Hispania.