Maziko ya aliyekuwa Baba wa Taifa la Zambia, Kenneth Kaunda yamefanyika katika makaburi ya viongozi wakuu wa nchi jijini Lusaka na kuhudhuriwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo, Edgar Lungu.
Mazishi yamefanyika ikiwa bado kuna taarifa zinazodai kuwa familia ya Hayati Kaunda haijakubaliana na kitendo cha serikali kuzika mwili huo badala ya kwenda kuuzika katika makaburi ya familia mahali alipopumzishwa marehemu mkewe, Betty.
Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Zambia, Abraham Mwansa jana alithibitisha kuwa maziko ya kiongozi huyo yangeendelea kama serikali ilivyopanga kutoka na kwamba Serikali haijapokea amri yoyote ya Mahakama ambayo iliitaka Serikali hiyo kutokuendelea na maziko hayo katika makaburi ya viongozi wa nchi hiyo.
Kaunda ambaye ni baba wa ukombozi wa nchi hiyo ya Zambia na baadhi ya nchi za kusini mwa Afrika alifariki dunia kwa matatizo ya upumuaji Juni 17, 2021 akiwa na miaka 97.