Kutokea kwenye kongamano la kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa inayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City DSM, Rais mstaafu Kikwete anazungumza muda huu katika hafla hiyo anasema anajivunia kuwa Mkapa Foundation alianzisha yeye akiwa madarakani.
Anaeleza kwamba Mkapa Foundation imesaidia sana kutengeneza miundombinu ya Afya na kuongeza wafanyakazi katika sekta hii na anaendelea kueleza jinsi taasisi hiyo ilivyosaidia Tanzania kenye mapambano dhidi ya UKIMWI na magonjwa mengine.
Rais Mstaafu Kikwete akiendelea kuelezea katika hafla hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City anasema alifanya n kazi na hayati Mkapa kwa karibu kwenye baraza la Mawaziri chini ya Rais wa wamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Baadae Mkapa akiwa Rais alimteua Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hapo ndipo walifanya kazi kwa karibu zaidi.
Kikwete anasema alipogombea Urais mwaka 2005, Mkapa alimuunga mkono na alipokuwa Rais, Mkapa alikuwa kati ya washauri wake wa karibu.
LIVE: RAIS SAMIA AKISHIRIKI KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA HAYATI RAIS BENJAMIN MKAPA -DSM