Ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi June 15, 2021 amefunguka kuhusu hali ya Afrika Kusini na kusema watanzania waishio nchini humo wapo salama na hakuna aliedhurika.
Ni baada ya kutokea kwa vurugu na maandamano yanayoendelea katika baadhi ya miji nchini humo ya kushinikiza kuachiwa kwa Rais Mstaafu Jacob Zuma.
‘Ndugu watanzania wenzangu kama ambavyo tumekuwa tukifuatilia kwenye vyombo vya habari baadhi ya maeneo hapa nchini Afrika Kusini yamekumbwa na machafu makubwa ambayo yamesababisha uporaji wa mali na uharibifu’- Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence
Maeneo yaliyokumbwa na vurugu ni Kwazulu Natal ambapo karibu ya watu mia tano wameshikiliwa na vyombo vya Usalama na watu kadhaa wamefariki, na hadi hivi sasa taarifa zinaonesha miji mengine mingi hali ni shwari-Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence
‘Vurugu hizi zilianza wiki iliyopita na zilianza kama Maandamano ya kupinga adhabu iliyotolewa kwa Rais Mstaafu Jacob Zuma ya kutumia kifungo cha miezi 15 ambayo alipewa na mahakama ya katibu hapa Afrika Kusini constitutional of court kama inavyojulikana mahakama ya juu’- Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence
‘Hata hivyo kadri siku zinazokwenda sasa maandamano hayo yamepelekea kusababisha uhalibifu wa Mali za watu na vifo vya watu’-Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence
‘Nichukue nafasi hii kufahamisha kuwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia ubalozi wetu hapa Pretoria hivi sasa haijapata taarifa kuhusu mtanzania yeye aliehusika katika vurugu hizo wala kifo, tunaomba watanzania wenzetu waliopo hapa Afrika Kusini wawe watulivu’- Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence
BALOZI AFRIKA KUSINI AWATOA HOFU WATANZANIA “HAKUNA ALIYEPATA MADHARA”