Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri katika Mabasi mawili tofauti kutoka Mbeya kwenda Tunduma wamejeruhiwa katika ajali ya Barabarani eneo la mlima Iwambi Barabara Kuu ya TANZAM majira ya saa mbili usiku.
Baadhi ya mashuhuda wamedai chanzo cha ajali ni mwendokasi na uzembe wa moja ya Mabasi hayo kujaribu kulipita basi jingine ndipo lilipopoteza mwelekeo kisha kuligonga basi jingine na yote yaliingia korongoni.
Taarifa za awali kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei eneo la ajali hakuna kifo chochote kilichotokea na idadi ya majeruhi bado haijafamika na ameelekea hospitali teule ya Ifisi ili kujua madhira ya abiria. Ulinzi umeimarishwa eneo la ajali chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi Debora Lukololo, updates zaidi kukujia.
MAHAKAMA YAKATAA MAELEZO YA SHAHIDI KWENYE KESI YA SABAYA “HAYAKUFUATA UTARATIBU”