Baada ya kuzuka kwa moto katika jengo la kituo cha kupokea, kupooza na kusambaza umeme cha Msamvu mapema leo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigela amezungumza na Vyombo wa Habari.
“Tumepata ajali ya moto katika kituo chetu kilichopo hapa Msamvu Morogoro kinachomilikiwa cha Shirika la Tanesco na kusababisha madhara katika kituo hiki pia kuleta madhara ya kukatika kwa umeme maeneo mengi ya Mkoa wa Morogoro”- RC Morogoro
“Nitoe pole kwa Tanesco kwa kuungua kwa kituo hiki na kipekee nawashukuru sana Vyombo vya Usalama kwa hatua ambayo wameichukua ya kudhibiti Moto ili madhara yasiyo makubwa zaidi”– RC Morogoro
“Hatua ambayo itakayofuata ni kwamba tutaunda kamati maalumu ambayo itakayohusisha vyombo vyote vya Usalama na Ulinzi pamoja na kushirikiana na Tanesco kubaini chanzo cha Moto”-RC Morogoro
AGIZO LA RC DSM ASEMA “MWANANCHI AKIKATAA KUVAA BARAKOA ASIPANDE GARI/NI AMRI SIO OMBI”