Kundi la Watalii 150 kutoka nchini Israel limetua katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo Agosti 2 alfajiri kwa ajili ya kutembelea hifadhi za taifa ambapo watalii hao ni sehemu wataliii 500 wanaotarajia kuingia nchini Tanzania.
“Tumepokea kundi la kwanza la watalii 150 kutoka Israel ni Soko kubwa la kiutalii Duniani na sasa inaonekana wameitambua Tanzania, wote tushikamane tuhakikishe hawa wageni wetu wakija basi wakiondoka wakaitangaze vizuri nchi yetu”- RC Arusha
“Mheshimiwa Rais wetu anatia mkazo kwenye kufanya nchi yetu ifunguke zaidi, Uchumi wetu uwe wa kisasa zaidi na Utalii mnajua ni Sekta yenye mchango mkubwa katika Uchumi wetu”-RC Arusha
TAZAMA RAIS SAMIA AKIWA ZIARANI NCHINI RWANDA “TUMEKUBALIANA KUENDELEZA USHIRIKIANO ULIPO”