Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kumruhusu Mbowe kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Katika shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya ambapo litatajwa Agosti 30, 2021.
Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kakosa la ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kuhusiana na mashtaka hayo, huku akieleza maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi.
Sambamba na madai hayo ya anadai haki zake kukiukwa kwa kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilisha kuwajulisha ndugu zake na wakili wake, pia Mbowe anadai kuwa wakati alipokwa ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa afisa wa polisi.
Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu, Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwawameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.