Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.
Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.
“Mimi sidhani kama mashtaka yamechochewa kisiasa kwasababu ninavyojua Mbowe alifunguliwa kesi mwezi wa tisa mwaka jana kwahiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashataka ni ugaidi na kuhujumu Uchumi nadhani wenzie kesi zao zimeshasikilizwa wengine wameshapewa sentensi zao wanatumikia”- Rais Samia
“Yeye upelelezi ulikuwa haujaisha Uchunguzi ulikuwa unaendelea kwahiyo amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi na tulipomaliza Uchaguzi nadhani sasa hivi Polisi tu wamekamalisha uchunguzi wao wamemuhitaji waendelee na kazi yao”- Rais Samia
“Na Kama utakumbuka Mbowe kipindi kirefu hakuwepo nchini alikuwepo Nairobi sasa kwanini kakimbia sijui, lakini alivyoingia tu Nchini akaitisha maandamano ya Katiba na madaia ya Katiba”- Mbowe
“Nadhani tuache Mahakamani zioneshe Ulimwengu kwamba hizo shtuma kama ni za kweli ama si za kweli basi Mahakama zitaamua”- Rais Samia
Video Courtesy: BBC Swahili
JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA 6 WALIOWAPIGA WATU WAWILI BAADA YA FUMANIZI