NI Agosti 20, 2021 ambapo waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi pamoja na Tozo.
Ayo TV iko mubashara muda huu unaweza ukabonyeza play kutazama kile kinachozungumzwa.
“Tangu makato ya tozo yaanze kwa hizi Wiki 4 hadi leo tumekusanya zaidi ya Bilioni 48, zaidi ya Bil 22 tulishapeleka kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), leo tumepeleka zaidi ya Bil 15 kwenye eneo hilohilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150”- Nchemba
“Kati ya hizi zaidi ya Tsh.Bil 48 tulizokusanya kwenye makato ya tozo kwa hizi Wiki nne, zaidi ya Bil 7 zimepelekwa kwenye madarasa, mtaona wenyewe tumepeleka fedha zijenge vituo 150 ambavyo vinaokoa maisha yetu, pia madarasa zaidi ya 500, ni Watoto wetu wanasoma”- Nchemba
“Ndani ya Wiki hizo nne za makato kwenye miaamala kwa miezi hii minne kwa upande wa Zanzibar wamekusanya Bilion 1.66, kwahiyo utaona jambo hili lina matokeo”—Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, Dar es salaam leo”- Nchemba