Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kuanzia leo August 23,2021 limeanzisha Operesheni dhidi ya magari yaliyosajiliwa kwa namba za Serikali STJ, STK, STL, DFP, SU, SM na mengineyo yote yanayoendeshwa bila kutii Sheria za Usalama Barabarani.
Nyigesa amesema imebainika baadhi ya magari hayo yanaendeshwa kwa mwendokasi kuyapita magari mengine pasipo kuchukua tahadhari na yana madeni makubwa yaliyotokana na tozo za papo kwa papo (Notification) na hawataki kulipa kwa hiari.
“Kumekuwa na tabia mbaya ya uendashaji vibaya kwenye Barabara ya Morogoro na Bagamoyo na nyingine zinazopita Mkoani Pwani, Watu wanaotumia magari ya STJ, STL, STK, PT, MT,SUM n.k wanaendesha bila tahadhari, nasema uendelee kutii sheria za Barabarani ukifanya makosa tutakukamata kama Mhalifu hata uwe na mkubwa ndani ya gari, wewe unamuita Boss wako sisi wote tutawaita Wahalifu maana hakukukemea”
“Operesheni hii ni endelevu na itagusa kila gari ambalo linadaiwa na linaendeshwa pasipo kutii sheria na alama za usalama Barabarani” ——— RPC Wankyo.
WAFANYAKAZI WATANO WA TRA WAFARIKI KWA AJALI WAKILIFUKUZIA GARI LILILODHANIWA KUWA NA MAGENDO
MWANZO MWISHO BASI LA SAULI NA LORI ZILIVYOGONGANA KIBAHA “DEREVA KA-OVERTAKE”