Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova leo Agosti 23, 2021 kwenye Amplifaya ya Clouds FM ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokua vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.
“Wakati mwingine Mtu akishafanya jambo flani anakuwa na hisia flani ambazo sio za kawaida labda anafikiri nikikaa hapa naweza nikadhurika, ni tatizo la kisaikolojia kwa Mtu ambae ana msongo wa mawazo anakuwa hajiamini na haamini Mtu yeyote yule, kwahiyo anaweza kufanya jambo lolote lile”- Kamand Mstaafu Suleiman Kova
“Mfano mimi zamani nilikua nahoji Wahalifu, akiletwa kwangu akisikia ni Kova anapoingizwa mule ndani anadondoka chini paap bila kumgusa, yani anaona amekutana na kitu cha hatari sana kutokana na yeye anavyoelewa, kama ni madhambi anayakumbuka yote” – Kamanda Mstaafu Suleiman Kova.
https://www.youtube.com/watch?v=OpuHfPIAoK4
TAZAMA ASKOFU GWAJIMA ALIVYOOMBA KUBADILISHIWA KITI, MIC ALIPOINGIA KUHOJIWA NA KAMATI, AOMBA ATUMIE DAWA KWANZA
ASKOFU GWAJIMA ALIVYOTINGA BUNGENI DODOMA KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI