Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa amefika mwenyewe katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa licha ya jana Kamati hiyo kutoa ombi kwa Spika wa Bunge Job, Ndugai akamatwe.
Silaa aliitwa kuhojiwa kwa mara ya kwanza katika kamati hiyo August 24, 2021 akituhumiwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Inaelezwa kuwa Mbunge Silaa alifika asubuhi na mapema kwenye viwanja vya bunge bila kusindikizwa na aaskari na kuelekea moja kwa moja kwenye ukumbi wa Spika na kuisubiri kamati.
KAMA ULIMISS ALICHOKISEMA MWENYEKITI JANA KUHUSU KUOMBA KIBALI KWA SPIKA NDUGAI ILI SILAA AKAMATWA NA KUFIKISHWA KAMATI YA MAADILI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA