NI Septemba 1 2021 ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba anazungumza na Waandishi wa habari muda huu kuhusu viwango vya tozo kwenye miamala vilivyopunguzwa.
“Wakati Rais anapokea kijiti kulikuwa na tarafa 217 hazina vituo vya afya, tukaweka malengo kwamba ukiweka na nyingine za kijiografia tukaenda target ya 220, makusanyo mpaka ya jana tunapeleka fedha nyingne kwa maana hiyo kwa Mwezi mmoja na nusu tumepata fedha za kujenga vituo 220 kwenye tarafa hizo ambazo zilikuwa hazina vituo vya afya tangu kupata uhuru sasa si mnaona hapo kwamba ni vema tu tuangalie viwango visituumize sana ila nia ya Rais ya kupeleka vituo vya afya kwenye tarafa zote ni nzuri”- Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba
“Vinajengwa vituo 220 tarafa zote na vina uwezo wa kufanya upasuaji, wodi za Wanawake na wodi za Watoto, tunakwenda kuokoa maisha ya Wanawake Wajawazito na Watoto”– Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba
“Kuna Watu wanapenda kujiita masikini lakini hawa waliopo vijijini wale masikini ndio Mama anakwenda kuwagusa wale ambao anaweza kupoteza maisha kwasababu hakuna Hospitali karibu nae, aliyepo Mjini anaweza kuchagua aende Hospitali ipi iwe za Serikali au Binafsi, anaweza kwenda Muhimbili akafika pale akasema ngoja niende Regency” – Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba
“Mama (Rais Samia) anasema sio tarafa tu hata kata ya kimkakati ambayo ipo mbali na huduma ya afya na yenyewe ipewe, tumemaliza vituo vya afya 220 fedha zipo na kuanzia sasa hivi pesa inayokusanywa kuanzia leo Mama ameagiza pesa ielekezwe kwenye madarasa na kwenye madawati Watoto wasikae chini”———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr.Mwigulu Nchemba, Dodoma leo
BREAKING: TOZO ZASHUSHWA, AGIZO LA RAIS SAMIA LATEKELEZWA,MWIGULU ATIA SAINI MAREKEBISHO YA KANUNI