NI taarifa kutoka mkoani Mtwara ambapo Kassim Joseph mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kijiji cha Namayakata anashikiliwa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia Muksini Namkwacha kwa Panga kisha kupelekea umauti.
Huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi baada ya Marehemu Muksini kulazimisha kupewa penzi na Dada yake Kassim au lasivyo apewe pesa zote alizompa.
Inaelezwa August 26 saa moja usiku Marehemu Muksini alikuwa na dada mmoja ambaye inasemekana kuwa ni Mpenzi wake na wakiwa kwenye mazungumzo walipishana lugha baada ya Muksini kumdai pesa zote alizowahi kumpa Mwanamke huyo kwa madai kwamba hataki kumpa penzi na ndipo kaka wa Mwanamke huyo aitwae Kassim Joseph alipoingilia kati na kumkata panga Muksin na kupelekea umauti.
RPC Mtwara Mark Njera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Marehemu alikuwa amelewa na kulazimisha aondoke na Mwanamke huyo au arudishiwe pesa zake.
RPC amesema Mwanamke aliyesababisha kifo amekimbia huku akiwataka Wananchi kuacha kujichukulia Sheria mkononi.
Ayo TV na millardayo.com imefika nyumbani kwa Marehemu unaweza ukabonyeza play kutazama kilichojiri nyumbani hapo.
MTU ALIYEGEUKA NYOKA MTWARA “ANALINDA KIJIJI, UKIMUONA HAULALI NI NYOKA WA AJABU”