Siku chache tangu kuuawa kwa Hamza na polisi August 25, 2021 baada ya kuwaua kwa risasi Askari watatu na mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amezungumza leo Mkoani Mwanza na kusema uchunguzi uliyofanywa na Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa Gaidi wa kujitoa mhanga.
“Kumekuwa na mambo yameendelea mitandaoni kwamba kwanini Polisi hawakumkata Hamza akiwa mzima ili kupata taarifa zaidi kutoka kwake, hilo Polisi walijitahidi matokeo yake wamejeruhiwa Polisi 6 na mpaka sasa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili”- DCI Wambura
“Suala la mapambano na Mtu mwenye silaha hilo huamuliwa na Askari aliye field ni wakati gani amkamate, amjeruhi au amuue, mapambano ya ana kwa ana kama ilivyokuwa kwa ishu ya Hamza tuwaachie Polisi, inashangaza kwamba pengine ilihitajika wafariki Askari zaidi ya watatu ndio Watu wangejua kulikuwa na umuhimu wa kumuua yeye”- DCI Wambura
“Kumekuwa ikisemekana kwamba Hamza alijisalimisha kwa kupiga magoti na kunyoosha mikono la hasha walioangalia ile clip vizuri Hamza hakujisalimisha, Hamza alipiga magoti baada ya kushambuliwa, tuna uhakika Polisi waliokuwa front line siku ile walifanya kazi nzuri”- DCI Wambura
“Imeendelea kusemwa kwamba Askari waliogopa kwamba Hamza angepona angeeleza mengi kuhusu Askari, hilo sio kweli, Hamza alikuwa Gaidi wa kujitoa muhanga hakuna ambacho Askari wangeogopa kwanza hakuna Askari ambaye alikuwa anamfahamu zaidi ya yeye kupora silaha na kuanza kuwashambuliwa na Hamza hakuwa Mtu mwema” —DCI Wambura
KWANINI HAMZA ALIWASHAMBULIA ASKARI PEKEE?, DCI AJIBU “MAGAIDI WANA CHUKI NA ASKARI”