Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewakabidhi eneo la Ujenzi Vikosi vya Ujenzi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Makabidhiano hayo yalifanyika Tarehe 30.09.2021 kwenye Makao Makuu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesema jengo hilo litakua la ghorofa sita na litajengwa kwa muda wa miezi 24.
“Mkandarasi atakayejenga jengo hilo ni Vikosi vya Ujenzi kutoka Wizara ya ya Ujenzi na Uchukuzi huku mhandisi mshauri akiwa ni Wakala wa Majengo Tanzania( TBA) na jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 23 ukijumuisha gharama za Mshauri” Shemdoe.
POLISI ALIVYOMZUIA DEREVA HUYU ASIENDELEE NA SAFARI “TUNAMSHIKILIA”