Unaambiwa Zaidi ya daladala 1,800 hazitoruhusiwa kufanya safari zake maeneo ya katikati ya jiji la Dar baada ya miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kukamilika na ujenzi huo wa miundombinu hiyo inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu ambapo mabasi 10 madogo na makubwa 20 yatatoa huduma za awali kama majaribio.
Meneja wa uendeshaji wa Dart Peter Mnuo amesema huduma hii ya majaribio inategemewa kutolewa December mwaka huu na huduma kamili itaanza kutolewa kuanzia July 2015 ambapo wakala wa mabasi hayo yaendayo haraka umekwishaanza maandalizi ya kutoa huduma ya awali ya mabasi makubwa kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni ikiwa kama sehemu ya mfumo wa kuanza kutoa huduma.
Mabasi hayo ya majaribio yanaweza kubeba jumla ya abiria 140 hadi 160 mpaka hapo itakapoanza kutolewa huduma kamili July 2015 ukiwa ni mradi uliopangwa kutekelezwa kwa awamu 6 ambapo kwa awamu ya kwanza unahudumiwa na fedha kutoka Benki ya dunia.