Bondia nyota nchini Salimu Jengo atapanda oktoba 13, 2021 kuwania mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Afrika (ABU) dhidi ya bondia Hannock Phiri kutoka Malawi.
Pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Light limeandaliwa na kampuni za Swahiliflix na Win Win Sports Promotion la uzito wa super light la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa Mtana uliopo kwenye jengo la Millenium Tower 2, Makumbusho, jijini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Win Win Promotion, Habib Halahala alisema kuwa kuwa mkanda huo upo wazi na kuamua kumpa nafasi Jengo ili kumtafutia nafasi ya kupenya kimataifa.
Mbali ya pambano hilo, kutakuwa na pambano la bondia nyota wa Congo Brazaville Adi Ndembo atapambana na Vincent Muziri katika uzito wa juu wa ABU.Pia bondia kutoka Afrika Kusini, Chriss Thompson atazichapa na Mganda Shafik Kiwanuka katika pambano la uzito wa juu.
Halahala alisema kuwa pambano hilo litaonyeshwa ‘live’ na mtandao wao wa Swahiliflix app ambayo inapatikana Google Play Store na vile vile kupitia Apple TV.
“Swahiliflix inayofuraha kuingia katika ngumi za kulipwa nchini kwa kushirikiana na wadau wengine kama Win Win Sports Promotion, Urban soul, Global Boxing Stars na Onomo hotel. Tunatarajia kuona mapambano makali nay a kusisimua kwani kila bondia amepania kushinda”>>> Halahala
Alisema kuwa mbali ya kuandaa mapambano, kampuni yao pia itasaidia kutoa ushauri ili kuendeleza vipaji vya ngumi za kulipwa kimataifa.
Alifafanua kuwa wamepania kufanya mambo makubwa katika ngumi za kulipwa hapa nchini kupitia mtandao wao wa kimataifa wa Swahiliflix.
Mbali ya mapambano hayo mawili, pia kutakuwa na pambano kali kati ya bondia kutoka Kenya Ryton Okwiri ambaye atapambana na bondia wa Uganda John Serunjogi ambapo bondia Joseph Sinkala atazichapa na Hamis Maya na Alex Kachelewa atapimana ubavu na Mwinyi Mzengela.
Kwa upande wake, Jengo alisema kuwa amejiandaa vyema kupambana na Phiri ambaye alikuja hapa nchini na kumchapa bondia Hannock Phiri kutwaa ubingwa wa WBF Afrika.