Oktoba 25, 2021 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ameagiza Taasisi ya Kilimo na Utafiti Mbeya (TARI) kuzirudisha kwa Wananchi wa Sae eneo la ardhi lenye hekali 67 ambalo lilichukuliwa na taasisi hiyo kinyume na sheria.
Waziri Lukuvi amechukua maamuzi hayo baada ya kufikishiwa kilio cha Wananchi hao kupitia kwa Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Tulia Ackson.
“Jambo hili nimeandikiwa sana lakini zaidi kwa kupitia Mbunge wa Jimbo hili la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amelisemea sana hadi Bungeni akitaka kujua hatma ya eneo hili lililochukuliwa na Taasisi ya TARI kwa Wananchi kinyume cha sheria”- Waziri Lukuvi
“Kumekuwa na ukiukwaji wa sheria katika maeneo mbalimbali hapa Nchini kwa watu au Taasisi kujichukulia ardhi ya mtu bila fidia tena sio fidia tu bali fidia stahiki”– Waziri Lukuvi
“Ninamaelekezo maalumu ya Rais Samia Suluhu ya kwamba Serikali yetu isisababishe taharuki kwa Wananchi wake, hili jambo la TARI kujichukulia eneo la Wananchi ni taharuki. Haiwezekani mkajichukulia eneo tena bila hata kuwalipa fidia na sasa natoa maelekezo kwamba eneo hili lirudishwe kwa Wananchi”-Waziri Lukuvi
Kwa upande wake Dkt. Tulia amesema>>>”Tunaishukuru sana Serikali yetu chini ya Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutusikiliza Wananchi kwa kilio chetu hiki ambacho kimedumu kwa miaka mingi bila utatuzi na leo suluhu imepatikana”
Wakati huohuo, Waziri Lukuvi ameagiza kusitishwa kwa muda shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika baadhi ya maeneo yanayodaiwa kuwa na makabuli ya wazee wa kimila yaliyopo eneo la Ituha hadi pale zitakapofanyiwa tasmini mpya.
KAMANDA AELEZEA THE CASK BAR KUTEKETEA MWANZA ” UCHUNGUZI WA KINA”