Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu imetupilia mbali pingamizi la Upande wa Utetezi la kutaka kutopokelewa kwa kielelezo cha Hati ya Ukamati wa mali katika kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga baada ya kupitia hoja za Mawakili wa Serikali na wa Utetezi, ambapo amesema anazipongeza pande zote mbili kwa kuibua hoja za Kisheria kwa sababu zinatoa mwanga kwa kufanya watu kujua namna ya sheria kama hizo kuwepo.
Jaji Tiganga amesema kuwa ni kweli Upande wa Mashitaka umewasilisha sheria ambayo sio sahihi, hivyo mahakama haiwezi kukubaliana na makosa hayo, lakini inaangalia kama kutakuwa na madhara indapo kielelezo hicho kikipokelewa.
Kutokana na hatua hiyo, Jaji Tiganga amesema anakipokea kielelezo hicho kwa sababu haoni madhara endapo kikipokelewa, hivyo shahidi wa nane ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Arumeru SP Jumanne Malangahe.
Pingamizi la Utetezi lilitokana na hoja wakipinga kielelezo hicho cha hati ya Ukamataji wa Mali kupokelewa na mahakama hiyo wakidai kimekiuka sheria.
Awali katika hoja zao Mawakili wa Utetezi akiwemo, Nashon Nkungu na wenzake wanapinga kupokelewa kwa Hati ya Ukamataji Mali ya Shahidi wa nane Kama Kilelezo cha Ushahidi kwa upande wa Jamhuri kwa madai kimekiuka matakwa ya Kisheria.
Wamedai Kuwa nyaraka hiyo imeandaliwa chuni ya kifungu cha 38( 3) ya mwaka 1985 sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018 shieria inayodaiwa kuwa haijawahi kufanyiwa mabadiliko mwaka huu wanaodai bali ilifanyiwa marekebisho 2019 hivyo haiwezi kuendana na sheria za Nchi.
Wamedai kuwa sheria hiyo waliotumia inafanya nyaraka hiyo kukosa nguvu ya Kupkelewa mahakani Hapo kwa haijulikani hivyo wanaomba mahakama Isipokee kama kielelezo cha Upande wa Jamhuri.
Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Mwandamizi Robert Kidando, amedai kifungu namba 20 (1) a, b, c cha tafsiri ya sheria sura ya kwanza ya mwaka 2019 ,sheria hiyo ipo hivyo haiwezi kusemwa kwamba nyaraka hiyo imetengenezwa katika sheria ambayo haipo.
Pia Kidando amedai katika mwaka 2018 kuna vifungu vya sheria ya CPA vilifanyiwa marekebisho ikiwemo mwengozo namba 7 wa mwaka 2018 ingawa haihusiani na kifungu 38 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Amedai katika mazingira hayo hatuwezi kusema kwamba sheria hiyo haipo katika vitabu vyetu vya sheria, hoja hiyo haipo, na kuna CPA moja tu nchini na sura 20 moja tu Tanzania bara, hata katika kesi walizozirejea haziendani na mazingira ya kesi hii
Alidai hatua waliyofikia ni kuona kama mahakama inaweza kupokea nyaraka hiyo na hakuna wakili hata mmoja kati yao anayelalamikia kama kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa upatikanaji wa nyaraka hiyo.
Ameendelea kutetea hoja yake kuwa sheria inayoongoza upokelewaji wa ushahidi mahakamani zipo wazi ikiwemo uhalali wa shahidi, nyaraka hiyo pia imerejea kifungu cha 35 sheria ya polisi inayompa askari Mamlaka ya kufanya upekuzi, hivyo wanaomba mapingamizi ya upande wa utetezi yatupiliwe mbali na nyaraka hiyo ipokelewe
Baada ya hija za Pande zote mbili shauri hilo limeahirishwa hadi hadi Novemba 9 ya mwak huu kwa ajili ya Kutoa uamuzi mdogo wa kwamba mahakama ipokee nyaraka hiyo kma kilelezo cha ushahidia Au lah.
Awali wakati akitoa ushanidi wake Amedai kabla ya kuwapekua alitafuta mashahidi ambapo aliwapata wanawake wawili na kwend nao aneo la tukio ambapo alianza kwa kujipekua yeye mwenyewe na kuwahakikishia mashuhuda kuwa hakuwa na kitu mwilini mwake na baadaye akaanza kumpekua Kasekwa ambaye alimkuta na silaha aina ya Bastola yenye namba A5340 pamoja na kete 58 za dawa zilizodhaniwa kuwa ni za kulevya.
Amedai upekuzi huo uliendelea kwa mtuhumiwa Lingw’enya ambapo alikutwa na simu kubwa aina ya Tecno ambayo ilikuwa na laini ya Halotel na Airtel na kete 25 za dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya.
Aliendelea kudai kuwa baada ya upekuzi vitu vyote vilijazwa kwenye hati ya ukamataji mali na kisha kusainiwa na wote watuhumiwa, mashahidi huru pamoja na yeye.
Amedai vitu vyote hivyo aliyopata katika upekuzi alimkabidhi askari mwenzake aliyemtaja kwa jina la Goodluck.
Baada ya maelezo hayo shahidi huyo aliweza kuitambua hati hiyo kulingana na vitu walivyojaza pamoja na saini walizoweka na mwishowe akaomba mahakama ipokee hati hiyo kama kielelezo katika mwenendo wa kesi hiyo na ndipo upande wa utetezi walipoibua pingamizi.