Barabara hii imeripotiwa mara kadhaa kutoka kwa abiria na wamiliki wa magari juu ya hali ilivyo hasa inapotokea mvua kunyesha eneo hili,taarifa niliyoipata ni kuwa kuna baadhi ya watu wamekwama toka juzi Mei 05 kutokana na ubovu wa barabara hii,kampuni za mabasi zimekua zikifaulisha abiria kutoka upande wa kwanza kwenda wa pili.
Ingawa bado kuna tatizo kwa baadhi ya wasafiri ambao walipanda mabasi ya kampuni zenye mabasi machache wamekwama toka Jumatatu,kuna taarifa ambayo sio rasmi kuwa Waziri wa Ujenzi Dokta John Magufuli anajiandaa kupeleka vifusi vya mchanga ili abiria waweze kupita na kuendelea na safari.
Barabara hii ndiyo inayounganisha sehemu mbalimbali kusini mwa Tanzania kama Mtwara,Lindi,Newala,Nachingwea,Masasi,Ndanda na Songea kwa watu wanaopitia barabara hiyo.
Cheki hali ilivyo.