Mexico City imetangazwa kuweka rekodi ya kuwa Jiji linaloongoza kwa kuwa na huduma ya Wi-Fi ya bure kwenye maeneo mengi, Guinness World Records imetangaza Jumatano wiki hii.
Guinness wanasema ukiwa Mexico City ambao ni Mji Mkuu wa Nchi ya Mexico ni kawaida kuona hadi Wi-Fi zaidi ya 2000 zikisoma kwenye simu au kompyuta yako na kila unayogusa inakubali bure tu , hapo ni wewe tu kujiachia na Internent .
Shule zilipofungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kupisha Corona baadhi ya Wanafunzi huduma hiyo iliwasaidia sana kusoma online.
Meya wa Mexico Claudia Sheinbaum amesema huduma hiyo imewekwa chini ya usimamizi wa Serikali katika eneo hilo kwa lengo la kupunguza gharama za maisha kwa Watu kununua mabando na kuwawezesha hata Watu wa kipato cha chini kuendelea kufurahia huduma ya kimtandao.