Hadi sasa Askari wenye silaha wako nje ya chumba cha Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta, Aishi Manula na Bakari Mwamnyeto hapa Le Centrall Hotel Antananarivo Madagascar wakitaka kuwachukua kwa nguvu kuwapeleka karantini, Uongozi wa TFF umekataa na pia umefanya Mawasiliano na FIFA pamoja na kuwafanyia vipimo vya tatu tena ambavyo wanasubiria majibu yake kabla ya mchezo wa mwisho dhidi ya Madagascar saa 16:00 EAT leo.