Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa Iringa leo amewapiga marufuku Madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa Wapangaji na kuwataka waache mara moja na badala yake pesa hizo walipwe na wenye nyumba.
“Tunawashangaa hawa majambazi wanaochukua kodi ya mwezi kwa Mpangaji, huu ni ujambazi kabisa, wewe unamtafutia fedha mwenye nyumba inakuwaje unachukua fedha kwangu kule nalazimishwa kulipa kodi ya Miezi 12 halafu kwangu unachukua kodi ya Mwezi mmoja, fikiria unapangisha appartment Masaki ya USD 400 unachukua kwa kazi ya Dakika moja halafu aibu huoni”
“Madalali wanaochukua pesa kwa Wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa wewe umeajiriwa na mwenye nyumba basi mwenye nyumba akulipe wewe, marufuku kumlazimisha anayepanga nyumba akulipe wewe”
“Tunaposema marufuku wasifikiri hatujui kufuatilia, Wananchi wanaotozwa hii namba yangu wanaijua, wala hauitaji sheria unahitaji common sense tu” ———Waziri Lukuvi