Kampuni ya Apple inapanga kuwapa Wateja wake wa simu, computer na vifaa vingine uwezo wa kutengeneza vifaa vyao wao wenyewe ikiwa ni baada ya shinikizo kutoka kona mbalimbali za dunia ambako Watumiaji wanataka apple wapunguze vizuizi vya kurekebisha vifaa vyao.
Kampuni hiyo Jumatano ilitangaza programu mpya ambayo itafanya vipuri vya bidhaa za Apple kupatikana ili kununuliwa kuanzia mapema mwaka ujao ambapo itawaruhusu Watumiaji kurekebisha vifaa vilivyoharibika kwa kutumia miongozo ya ukarabati ambayo Apple itaiweka kwenye tovuti yake.
Kwa sasa programu hii ya ukarabati itapatikana tu kwa Watumiaji wenye iPhone 12 na iPhone 13 lakini baadaye itapanuka hadi kwenye kompyuta za mac zinazotumia chipu mpya ya Apple ya M1.