Gavana wa Oklahoma Kevin Stitt amemuhurumia Mfungwa Julius Jones na kubatilisha hukumu ya kifo ya Jones saa chache kabla ya kunyongwa kwake kutokana na mauaji anayodaiwa kuyafanya mwaka 1999 japo mwenyewe amekua akisema hakuyafanya.
Hukumu ya Jones ambaye alikua anyongwe saa nne asubuhi itabadilishwa na sasa itakuwa kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa kuachiliwa huru, Hukumu yake ya kifo imekua ikipingwa na Mastaa kadhaa waliopaza l sauti ili Gavana wa aibatilishe, mastaa hao ni pamoja na Kim Kardashian, Mwigizaji Kerry Washington, Mandy Patinkin na hata Wanamichezo akiwemo Beki wa Timu ya Cleveland Browns, Baker Mayfield.
Anayedaiwa kuuwawa huo mwaka 1999 ni Howell ambaye aliuawa katika utekaji nyara wa gari usiku wa saa tatu na nusu ambapo wakati huo Jones alikua na umri wa miaka 19 na alikamatwa siku moja baada ya Mamlaka kupata silaha iliyotumika kwenye mauaji ikiwa imefungwa kwenye nguo nyekundu ndani ya nyumba ya familia yake.